In Summary

•Kupitia Instagram, Otile alisema kwamba alikuwa akitafuta mwimbaji wa kumshauri, na kuongeza kuwa anaweza kuwa kutoka sehemu yoyote ya Kenya.

•Alisisitiza umuhimu wa kufahamu  lafudhi ya lugha hiyo, akitaja kuwa ni muhimu sana kwa nyanja ya muziki.

otile Brown
Image: instagram

Mwanamuziki mashuhuri Otile Brown ameahidi kumnoa mtu mmoja nchini Kenya ambaye ana talanata ya kuimba nyimbo za Kiswahili.

Kupitia Instagram, Otile alisema kwamba alikuwa akitafuta mwimbaji wa kumshauri, na kuongeza kuwa anaweza kuwa kutoka sehemu yoyote ya Kenya.

Zaidi ya hayo, Otile alisisitiza kwamba msanii anapaswa kuwa na umuhimu wa kuimba kwa Kiswahili.

Alisisitiza umuhimu wa kufahamu nuances na lafudhi ya lugha hiyo, akitaja kuwa ni muhimu sana kwa nyanja ya muziki.

"Natafuta msanii wa kike anayekuja wa kushauri.”

“Unaweza kuwa kutoka sehemu yoyote ya Kenya mradi tu unajua kuimba Kiswahili kizuri. Rafudhi ni muhimu kwenye nyimbo zetu za kiswahili,” Otile alisema.

Kauli za Otile zinakuja saa chache baada ya kuachia wimbo mpya wa Kiswahili unaoitwa ‘Furukuta’.

Hivi majuzi baada ya maandamano kushuhudiwa nchini Otile alijibu vikao vilivyopendekezwa na Rais kuwa ni ufujaji wa rasilimali na kutaka uwajibikaji kutoka kwa maafisa wa serikali.

“Tatizo tunapenda kupoteza mUda na rasilimali nyingi kwa maneno, maneno matupu huleta hasara, maongezi ya nini tena?? We all got job to do, kila mtu afanye kazi yake na wajibike.Sote tunajua cha kufanya,” Otile aliandika.

Mwimbaji huyo aliangazia haja ya kukabiliana na ufisadi, ambao aliutaja kuwa ni upotevu mkubwa wa fedha za umma, na kusababisha hasara nyingi.

“Tujifunze vizuri kusimamia nchi na mali, ufisadi umezorotesha maisha ya mwananchi ata wawekezaji wanatoroka, kazi zina pungua.

View Comments