In Summary

• Rema alifichua kwamba alitiwa moyo na waimbaji wakubwa wa Afrobeat kama vile Don Jazzy, Mo’hits crew, 2Baba, Olamide, P-Square, na Timaya kwa albamu yake ya pili, ‘HeIs’.

Rema adokeza pesa zake za kwanza alimpa mamake zote.
Image: Instagram

Mwanamuziki Rema kutoka Nigeria amewashauri wenzake katika tasnia ya muziki kuhifadhi na kusherehekea utamaduni wa Afrobeat nchini humo badala ya kukumbatia mtindo wa Amapiano ambao asili yake ni Afrika Kusini.

Rema alisisitiza umuhimu wa kuendeleza athari za Afrobeats kwenye mandhari ya muziki wa Kiafrika, akitaja ushawishi unaokua wa Amapiano katika tasnia ya muziki ya Nigeria.

Rema alitambua amapiano kama aina nzuri katika mahojiano ya hivi majuzi na Apple Music lakini alisisitiza umuhimu wa kuweka sauti na ushawishi tofauti wa Afrobeats.

Rema alifichua kwamba alitiwa moyo na waimbaji wakubwa wa Afrobeat kama vile Don Jazzy, Mo’hits crew, 2Baba, Olamide, P-Square, na Timaya kwa albamu yake ya pili, ‘HeIs’.

Alipongeza mtindo wa kipekee wa utayarishaji wa Afrobeat, ambayo anaamini inaweza kutawala vilabu vya Kiafrika, na kuwahimiza wasanii wenzake kuendelea kutoa muziki wa hali ya juu wa afrobeat.

Kwa maneno yake:

"Ilinibidi nirudi nyuma [wakati nikitengeneza albamu yangu mpya]. Nilipata msukumo mwingi kutoka kwa Mo’hits. Kwa sekunde nne za kwanza, wimbo wa Mo'hits unapoingia, tayari unajua ni wimbo wa Mo'hits. Don Jazzy anaserereka kwa mdundo huo.”

“Kipindi ambacho Olamide alikuwa akiachia nyimbo za vaibu, bado anaachia nyimbo za kuvutia. Wakati ambapo wimbo wa Olamide unakuja bado unajua. P-Square, 2Face, au Timaya. Kulikuwa na nyakati ambapo beat tu.”

"Amapiano ni nzuri, ni moto lakini kulikuwa na wakati ambapo uzalishaji wa Afrobeats ulikuwa wa kichaa sana kwamba hakuna kinachoweza kuishi katika vilabu vya Afrika. Sisemi kwamba tumepoteza hilo lakini ninasema tu kwamba tunahitaji zaidi ya hayo. Sitaki twende mbali sana na hilo. Tunahitaji kuiendeleza.”

View Comments