In Summary

• Chege na Dibul wamekuwa wakichumbiana kwa zaidi ya miaka miwili na walianza kuishi pamoja mwezi Julai mwaka jana, 2023.

DJ DIBUL NA DOREA CHEGE
Image: INSTAGRAM

Mwigizaji wa zamani katika kipindi cha Maria kwenye runinga ya Citizen, Dorea Chege kwa mara ya kwanza amezungumzia uvumi ambao kwa muda umekuwa ukienezwa mitandaoni kuhusu sababu ya yeye kutokuwa na mtoto na mpenzi wake.

Chege ambaye alipata jina la ‘Maggie’ alipokuwa akiigiza katika kipindi hicho miaka minne iliyopita alisema kwamba kwa muda amekuwa akiburuzwa mitandaoni na tetesi za uongo wengine wakiibua dhana za kujibu sababu yake kutomzalia Dj Dibul mtoto licha ya kuchumbiana kwa muda.

Chege na Dibul wamekuwa wakichumbiana kwa zaidi ya miaka miwili na walianza kuishi pamoja mwezi Julai mwaka jana, 2023.

Akizungumza kwenye kipindi cha Love in the Wild kinachoongozwa na Dj Mo na Size 8 kwenye runinga ya TV47, Chege alisema kwamba amekuwa akiona baadhi wakizua uvumi kwamba aliwahi pata mimba lakini kwa bahati mbaya ikaharibika.

Mrembo huyo alikanusha uvumi huo na kusema kwamba hajawahi pata mimba na wala hajawahi haribikiwa na mimba, akiwataka watu kutompa shinikizo mitandaoni kuhusu ni lini atamzalia Dibul.

“Ni kweli kuna presha napatiwa mitandaoni, na kuna maoni niliona mahali watu wakisea ‘ooh Dorea zalia Dibul’ halafu nikaona mwngine akijibu ‘eeh hapana msimpe presha alipoteza mimba’. Nilishangaa nilipoteza mtoto lini?” Chege alisema.

“Kuna wengine wanasema mimi nimepata watoto 3 ndani ya mwaka mmoja, hilo linawezekanaje? Watu wangu, mimi sijawahi poteza mtoto wala sijawahi pata mimba. Mtulie, kakiingia lazima tutawaambia,” aliongeza.

Akimtetea dhdi ya tetesi hizo, Size 8 aliwashauri watu kwamba si kila kitu wanachokiona kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maisha ya maceleb ni cha kweli.

Size 8 aliwaambia watu kama wanataka kufahamu ukweli, ni vyema kutembelea akaunti rasmi za watu husika katika mitandao ya kijamii.

View Comments