In Summary

• Katika ujumbe huo wake, watu mbalimbali walianza kumtania wengine wakimwambia kwamba alikuja bila kutoa taarifa ili aarifiwe mapema kuhusu hali ya hewa Nairobi.

 

CHRISTINA SHUSHO

Msanii wa Injili kutoka Tanzania, Christina Shusho yumo nchini Kenya kwa ajili ya mkutano wa injili utakaofanyika baadae Jumamosi jijini Nairobi.

Baada ya kutua jijini Nairobi, Shusho alipigwa na butwaa na kile alichokitaja kuwa ni utofauti mkubwa wa hali ya anga kati ya Nairobi n Dar es Salaam.

Msanii huyo alisema kwamba Nairobi kulikuwa na baridi kali kuliko kule alikotoka na kuteta kwa utani akihoji kwa nini mashabiki wake wa Kenya waliokuwa wanajua kuhusu ujio wake hawakumuambia.

“Mbona hamkuniambia Nairobi kuna baridi hivi?” Shusho aliuliza.

Shusho aliwakaribisha Wakenya wote walioko jijini Nairobi kwa shoo hiyo majira ya saa tisa alasiri ambayo itaongozwa na mtangazaji nguli Maina Kageni.

“Je, uko karibu na Thika Grove Chania kando ya Barabara ya Gatanga? @FinscoAfrica, @ItsMainaKageni na mimi tuna kitu maalum leo. Njoo tukutane na Tuzungumze. Nitatumbuiza saa 3 jioni. Kuingia ni Bure,” aliongeza.

Katika ujumbe huo wake, watu mbalimbali walianza kumtania wengine wakimwambia kwamba alikuja bila kutoa taarifa ili aarifiwe mapema kuhusu hali ya hewa Nairobi.

Jijini Nairobi, msimu wa baridi kali umekuwa ukihanikiza katika maeneo mengi hswa mwezi wa Julai.

View Comments