In Summary

• “Bado wanategemeana japo kuna vitu Fulani labda hatutamuona Alikiba Wasafi au Diamond Crown kwenda kufanya mahojiano" alisema Lokole.

alikiba na diamond

Mtangazaji wa kituo cha habari cha Wasafi, Juma Lokole amefunguka kwamba hakuna uadui uliopo baina ya Alikiba na Diamond licha ya dhana hiyo kujijenga kwa mashabiki kwa miaka mingi sasa.

Akizungumza na blogu moja nchini humo, Lokole alisema kwamba kama ni uhasama unaishia kwenye muziki lakini likija suala la kibiashara, Alikiba na Diamond wote wanategemeana pakubwa.

“Upinzani unabaki kwenye miziki yao tu wanayofanya. Ukishakuwa mkurugenzi kwenye taasisi Fulani basi hutakiwi kuweka misingi kwenye sehemu moja. Kwa Alikiba kusema labda kumuongelea vizuri Diamond kwenye mahojiano anayofanya na unajua wazi wana tofauti zao, ndio maana hata Diamond mwenyewe akiwa anamuongelea Alikiba, humkuti anamuongelea vibaya kwa sababu wote wanategemeana.”

“Bado wanategemeana japo kuna vitu Fulani labda hatutamuona Alikiba Wasafi au Diamond Crown kwenda kufanya mahojiano lakini inapofika tunahitajiana kwa sababu Crown watahitaji stori zetu ili mambo yaende na sisi tutawahitaji wao pale inapotokea stori zao mambo yaende. Kwa hiyo tunaishi kwa kutegemeana,” Juma Lokole alieleza.

Kuhusu iwapo siku moja atafikiria kuihama Wasafi kwenda Crown ya Alikiba, Juma Lokole alisema kwamba hakuna lisilowezekana bali ataangalia maslahi kwanza na akipata dau nono kule bila shaka hawezi kata.

View Comments