In Summary

• Hata hivyo, ni vizuri kufahamika kwamba Kiengei baada ya kufikwa na maji shingoni, alinywea na kuomba radhi kwa matamshi ambayo huenda yalimkera Pritty Vishy na wanawake wengine.

• Ni msamaha ambao Pritty Vishy alikataa katakata kuukubali akisema mchungaji huyo alifanya hivyo kwa makusudi.

 

PRITTY VISHY NA PASTOR KIENGEI
Image: INSTAGRAM

Kufuatia video ya mchekesaji ambaye pia ni mchungaji Muthee Kiengei akikejeli Pritty Vishy kwa maumbile ya mwili wake kusambaa mitandaoni, baadhi ya wanawake maarufu nchini Kenya wamevunja kimya chao.

Wanawake wengi walionekana kukereka na video hiyo wakihisi mchungaji Kiengei si tu alimkosea Pritty Vishy bali pia aliwakosea wanawake wote na pia Mungu kwa kukosoa uumbaji wake katika mwili wa Vishy.

Rapa Femi One aloichukua kwenye ukurasa wake Instagram na kuonyesha hasira zake dhidi ya mtumishi wa Mungu akimsuta kwamba alikosa kumkejeli Vishy ambaye hata hawajawahi kufarakana hapo awali.

Femi One anahisi kwamba ni wakati Wakenya wawe na mjadala pevu kuhusu watu ambao wanastahili cheo cha kuitwa wachungaji na maaskofu, kwani wengine hawastahili hata kidogo.

“Video hii iliyofanywa ilinikasirisha kwa viwango vingi sana. Huyu ni Askofu na Jumapili kuna uwezekano mkubwa atakuwa anahubiri jinsi sisi sote tumeumbwa kwa sura ya Mungu!! Na huyu Host anacheka cheka nini …such an enabler . Na utani huo rahisi wa mvulana…Inasikitisha kusema kidogo. Ni wakati muafaka wa kuwa na mazungumzo ya uaminifu kuhusu makasisi katika nchi hii,” Femi One alisema kwa hasira.

Mwingine aliyeonyesha kukerwa na video hiyo ni Nana Owiti, mke wa rapa King Kaka.

Owiti alisema kiwamba moyo wake ulizama kwa hasira kuona mwanamume ambaye husimama kwenye mimbari kuhubiri kuhusu upendo wa Mungu akiwabagua hadharani baadhi ya watu kisa mionekano ya miili yao.

“Nilitazama video hii na moyo wangu ukafadhaika. Ni vigumu kuamini lakini mwanamume huyo ni kasisi-mtu ambaye husimama juu ya mimbari kila Jumapili akihubiri kwamba tumeumbwa kwa mfano wa Mungu lakini hapa anamrarua Pritty Vishy-mwanamke mdogo ambaye kwa ujasiri na kwa hatari ameshiriki mapambano yake na kujithamini,” Nana Owiti alisema.

Hata hivyo, Karen Nyamu alionekana kupuuza kelele za Vishy na kusema kwamba kejeli hizo ni kidogo na kumtetea Kiengei akisema tayari ameshakiri makosa na kuomba msamaha.

Nyamu alionekana kusimama na mchungaji Kiengei kwa dhana kwamba Pritty Vishy amewahi mtukana mtandaoni siku za nyuma.

“Leo analia kwa sababu ya kauli nyepesi zinazotolewa juu yake. Ndio nilisema nyepesi. Najua Askofu ni mcheshi. Lakini kupata uhakika wake. Anataka Vishy achukue mtafaruku au jambo la kujulikana kuhusu n si tu uhusiano wake na Simple Boy. Ikiwa anaweza kupata ukweli huo anaweza kujiboresha,” Seneta Nyamu alisema.

Hata hivyo, ni vizuri kufahamika kwamba Kiengei baada ya kufikwa na maji shingoni, alinywea na kuomba radhi kwa matamshi ambayo huenda yalimkera Pritty Vishy na wanawake wengine.

Ni msamaha ambao Pritty Vishy alikataa katakata kuukubali akisema mchungaji huyo alifanya hivyo kwa makusudi.

 

View Comments