In Summary

• Wiki moja iliyopita, Huddah alikuwa amempa Salasya masharti kadhaa ya kukidhi iwapo alikuwa anataka kumpa mwaliko wa kukutana.

HUDDAH NA SALASYA
Image: HISANI

Mwanasosholaiti Huddah Monroe amezungumzia uwezekano wa kukubali kuolewa na mbunge wa Mumias Mashariki, Peter Salasya.

Huddah aliweza wazi hisia zake kuhusu majaribio kadhaa ya Salasya kumnyemelea, alipokuwa akijibu maswali ya mashabiki wake wakati aliandaa kipindi cha maswali na majibu kupitia Instagram siku moja iliyopita.

Kutokana na kutaniana kati yake na Salasya ambako kumejiri katika siku za hivi karibuni, mashabiki wengi walimrushia maswali wakitaka kubaini uhusiano wake na mbunge huyo mcheshi na kama atamkubalia kuwa mpenzi wake endapo atapata nafasi kama hiyo.

“Unaweza kubali kuolewa na Salasya,” mmoja alimuuliza.

Akijibu, Huddah alimsifia Salasya kama mtu mcheshi muda wote na kusema kwamba hatojali kuwa mke wake.

“Ni mtu wa ajabu sana, anapenda kucheka muda wote. Ni mtu mwenye furaha saa ishirini na nne kwa wiki, mbona nisikubaliu,” Huddah alijibu.

Kuhusu kumvunja moyo, Huddah alisema kwamba hawezi fikiria hata ku8mvunja moyo kwa sababu anavyomjua mbunge huyo, hatostahimili.

Hivi majuzi, mbunge huyo alidokeza kwamba alikuwa katika awamu ya lala salama kujiandaa kukutana na Huddah lakini akaomba mashabiki wake usauri jinsi ya kukutana na mwanasosholaiti huyo ghali.

Wiki moja iliyopita, Huddah alikuwa amempa Salasya masharti kadhaa ya kukidhi iwapo alikuwa anataka kumpa mwaliko wa kukutana.

“Also sitaki story ya isukuti kwa airport. niko faragha. Naingiaga na ninja meeting zangu ni JW Marriott. Chumba cha rais… kimejaa waridi za machungwa. Salama na dola 30,000 za salamu ama sitaongea muda wote,” alisema.

View Comments