In Summary

• Khalif Kairo amefanya vyema katika mitihani ya kupaa ndege za abiria.

khalif Kairo
Image: Instragram

Mshawishi wa mtandaoni na mfanyabiashara  Joseph Wambui Kairu maarufu kama Khalif Kairo amesherehekea mafanikio yake ya kufanya vyema katika mtihani wa urubani.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Kairo amebandika picha ya hati ya matokeo ya mtihani wa mamlaka ya usafiri wa anga ya Kenya KCAA ambao amefanya vyema katika kila somo.

Wengi wa wafuasi wake wamepokea taarifa hizo kwa hisia mseto wakimhongera na wengine wakituma jumbe za utani. Ijapokuwa wengi wamemhongera kuwa rubani, hati aliyopata Kairo si leseni ya kumfanya rubani bali matokeo yake yatadhibitishwa kabla ya kukabidhiwa leseni.

Baadhi ya jumbe alizopokea Kairo ni:

"Naona umebakisha sasa flying license uanze kuinua aviator ka mimi." alisema Mass Servant.

"Kumbe huyu jamaa mmekuwa mkimpiga mawe mawe amekuwa classes.. thought it was hire to move his girls around." alisema Emoji.

"Yaani hakuna kitu umefikisha 90%." alisema Helter Skelter.

Matokeo kwenye hati ya Khalif ni halali kwa muda wa miezi kumi na minane pekee.

 

View Comments