In Summary

• Msanii huyo alifichua kwamba kabla ya kufunga ndoa na Nameless mwaka 2005, walikuwa wamechumbiana kwa miaka minane.

 
• Kwa hiyo ni sahihi kusema kwamba mahusiano ya wawili hao wenye umaarufu mkubwa yamedumu kwa miaka 27 sasa.

NAMELESS NA WAHU
Image: INSTAGRAM,

Wasanii Nameless na Wahu wamesherehekea miaka 19 tangu walipofunga harusi yao rasmi na kuwa mke na mume.

Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, Nameless na Wahu walichapisha msururu wa picha wakisherehekea mlo mtamu na kuachia ujumbe wa jinsi maisha yao yamekuwa ya kufana katika miongo miwili iliyopita.

Kando na kuwa mke wake, mama kwa mabinti wake watatu, Nameless alimtaja Wahu kuwa mshirika wake wa maisha ambaye pia ni msiri wake wa milele.

“Leo tunaadhimisha miaka 19 tangu tuseme "I DO" ! Kwa rafiki yangu bora, mpenzi wangu, na mshirika wa maisha! Tuendelee kukua na kujifunza pamoja! Heri ya kumbukumbu ya miaka Babe! Nakupenda daima na milele️! Hapa kuna mengi zaidi! Na kwa familia zetu mtandaoni, asante kwa kutuonyesha upendo kila wakati na kuwa sehemu ya safari yetu!” Nameless aliandika.

Mwaka juzi wakisherehekea miaka 17 ya ndoa, Wahu alipakia video akionesha jinsi walikuwa na tafrija ya kitamaduni baada ya harusi.

Video hiyo ilionyesha Wahu akiwasili kwenye ukumbi wa harusi kwa mashua, akiwa amevalia nguo nyeupe na ngozi ya mnyama ya kahawia.

Msanii huyo alifichua kwamba kabla ya kufunga ndoa na Nameless mwaka 2005, walikuwa wamechumbiana kwa miaka minane.

Kwa hiyo ni sahihi kusema kwamba mahusiano ya wawili hao wenye umaarufu mkubwa yamedumu kwa miaka 27 sasa.

View Comments