In Summary

• Awali, YouTuber huyo alitikiza mitandao ya kijamii baada ya kutangaza kuvunjika kwa uhusiano wao, siku tatu tu baada ya kumsherehekea Shiru kwa ujumbe mtamu siku yake ya kuzaliwa.

FELICITY SHIRU NA THEE PLUTO
Image: INSTAGRAM

YouTuber Thee Pluto amesisitiza kwamba kuvunjika kwa ndoaq yake na Felicity Shiru si kiki bali ni jambo ambalo lilijiri kweli.

Pluto kupitia instastory yake, alisema kwamba kuna baadhi ya watu walihisi ni kiki wanafukuzia, saa chache baada ya kutangaza kuwa uhusiano wake na Felicity Shiru ambao ulikuwa umedumu kwa miaka 3 ulilazimika kufikia mwisho.

Japo alikiri kwamba kuna ujio wa video ya wimbo ambayo walishiriki pamoja na ambayo itatoka hivi karibuni, lakini alisema kwamba hilo halina chochote kuhusiana na kuachana kwao, kwani video ilishafanywa na kutayarishwa awali hata kabla ya tofauti zao katika klabu kujiri.

“Hakuna kitu chochote cha kufanyia mzaha kuhusu taarifa niliyotoa awali, ni kweli kuna muziki unakuja lakini hilo ni suala lingine kivyake na tulishafanya video tayari. Kuhusu kuachana, sifanyi mzaha, ni kweli tumeshaachana,” Pluto alisisitiza.

Awali, YouTuber huyo alitikiza mitandao ya kijamii baada ya kutangaza kuvunjika kwa uhusiano wao, siku tatu tu baada ya kumsherehekea Shiru kwa ujumbe mtamu siku yake ya kuzaliwa.

‘Tumeamua kila mmoja kufuata njia yake na hivyo kufikisha mwisho uhusiano wetu uliodumu kwa miaka mitatu. Ahsante kwa sapoti yenu kutoka kwa familia, marafiki na mashabiki. Hebu na tusije tukaanza kushuku chochote na kuanza kusambaza uvumi usio wa kweli kuhusu utengano wetu,” Thee Pluto alitangaza.

Aidha, baba huyo wa mtoto mmoja wa kike, Zoey alisema kwamba licha ya kutalikiana, wataendelea kushirikiana sako kwa bako kwa ajili ya maleiz ya binti wao.

“Tutaendelea kushirikiana vizuri kwa ajili ya malezi ya binti wetu ili asije akathurika. Tupeni muda wakati huu tunapitia mgumu, ahsanteni,’ Pluto alimaliza.

 

View Comments