In Summary

• Kwa mujibu wa Pozee, jambo hilo ndilo lilimpotezea fursa ya kipekee ya kufanya kolabo na mshindi wa Grammy kutoka Nigeria, Wizkid miaka minne iliyopita.

• “Niko na wimbo mkubwa kabisa kwa sasa ‘kuukuu’ uliotoka miezi 5 iliyopita, acheni kuunga mkono watu-baki, sapoti talanta za kweli na muziki wa kweli.”

Image: INSTAGRAM

Msanii Willy Paul ameelezea mazingira yaliyopelekea fursa adimu kutoweka mikononi mwake miaka minne iliyopita ya kufanya kolabo na mkali kutoka Nigeria, Wizkid.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Willy Paul alisema kwamba anahisi wasanii wa Kenya wengi wao wanapaishwa zaidi kuliko uwezo wao kimuziki.

Msanii huyo wa Saldido alisema jambo hili la kuwapaisha wasanii wa Kenya kinyume na kile ambacho wana uwezo wa kufanya ndilo linaua tasnia ya muziki wa Kenya.

“Wasanii wengi wa Kenya ni kama tu wanapewa sifa kupita kiasi. Na huo ndio upuuzi mkuu unaoua tasnia ya muziki Kenya,” Pozee alisema.

Alisema kwamba wimbo wake uliotoka miezi 5 iliyopita ndio wimbo mkuu humu nchini lakini watu wamepata fahari katika kusifia nyimbo zisizo na maana kuliko kusifia nyimbo za maana kama wimbo wake.

Kwa mujibu wa Pozee, jambo hilo ndilo lilimpotezea fursa ya kipekee ya kufanya kolabo na mshindi wa Grammy kutoka Nigeria, Wizkid miaka minne iliyopita.

“Niko na wimbo mkubwa kabisa kwa sasa ‘kuukuu’ uliotoka miezi 5 iliyopita, acheni kuunga mkono watu-baki, sapoti talanta za kweli na muziki wa kweli.”

“Kwa muda mrefu sasa wasanii wa kimataifa wamekuwa wakidanganywa, wanaaminishwa kwamba mtu mwenye watu Fulani ndiye mkubwa, nilipotreza fursa ya kufanya kolabo na Wizkid kwa sababu ya suala lili hili miaka 4 iliyopita. Sijawahi zungumzia hilo lakini watu wenyewe wanajijua,” Pozee alilalamika.

Hata hivyo, msanii huyo alisema kwamba anamshukuru Mungu kwani sasa hivi hadithi zimebadilika na yuko mbioni kuteka anga za muziki katika majukwaa ya juu zaidi.

View Comments