In Summary

• “Same sounds, the same genre...tunahitaji diversity and originality,” shabiki huyo alimwaambia.

KHALIGRAPH JONES
Image: INSTAGRAM

Rapa matata wa humu nchini Khaligraph Jones ametoa jibu lenye uchachu wa aina yake kwa shabiki mmoja aliyeonekana kusuta mtindo wake wa uimbaji.

Jones alidokeza kwamba zilikuwa zimesalia saa chache kabla ya yeye kuachia muziki mpya kwa jina Billionaire.

Shabiki huyo alifika kwenye upande wa kutoa maoni na kumfokea akisema kwamba anazungumza kwa niaba ya mashabiki wa Jones wote ambao wanadai kuchoka na mtindo wake mmoja tu wa kuimba.

Shabiki huyo alimshauri Khaligraph Jones kuzingatia kujaribu mitindo mingine ya kufoka akisema mashabiki wanahitaji ladha tofauti kutoka kwake.

“Same sounds, the same genre...tunahitaji diversity and originality,” shabiki huyo alimwaambia.

Hata hivyo, Khaligraph Jones alimuona shabiki huyo kama mpuuzi na kumfokea akimwaambia kuwa yeye ni msanii wa rap na hiphop wala si wa miziki kama ya wasanii kutoka Ukambani.

“Wewe ni ngombe, sasa unataka niimbe katitu? Hapa ni Rap Hip Hop baba,” Khaligraph alimjibu shabiki huyo.

Papa Jones, kama anavyojiita kwa jina la majazi ametajwa kama mmoja wa wasanii wa muziki aina ya rap ambao wameleta mwamko mpya na kubadilisha dhana mbaya iliyokuwa inahusishwa na aina hiyo ya muziki kwa muda mrefu humu nchini.

Kupitia kwa rap, Jones amefanikishwa kujenga jumba la kifahari na pia kupata nafasi ya kushiriki katika majukwaa makubwa na wasanii tajika.

Wiki iliyopita, Jones alipata nafasi adimu ya kushiriki kwenye jukwaa moja na wasanii tajika katika tamasha la kuombea nchi ya Haiti Amani na utulivu.

Tamasha hilo liliandaliwa na serikali ya Kenya kupitia wizara ya mambo ya nje ambapo lengo lilikuwa kuomba utulivu nchini Haiti ambako maafisa wa polisi kutoka Kenya zaidi ya 500 wametumwa kujaribu kuleta hali ya utulivu katika mitaa ya mji mkuu wa Port-au-Prince

View Comments