In Summary

• Awali katika klipu iliyowatia huruma wengi, mama mzazi wa Bradley alihojiwa akikiri kwamba mwanawe aliacha kuchukua simu zake tangu umaarufu kumjia mwezi mmoja uliopita

BRADLEY
Image: FACEBOOK

Bradley Marongo maarufu kama Gen Z Goliath kwa mara nyingine amesisitiza kwamba madai ya mama yake kwamba tangu apate umaarufu aliitelekeza familia yake ni uongo.

Akijibu mipigo siku moja tu baada ya mamake kufanya mahojiano yaliyosambaa akidai mwanawe kuwatelekeza hata kutopokea simu zao kutoka nyumbani, Marongo alisema kwamba yeye huwapigia simu na hata kuwatumia hela za matumizi.

Kijana huyo anayetajwa kuwa mrefu zaidi humu nchini alidai kwamba shida kuu ya mama yake ni kutaka asafiri naye kila mahali anapokwenda, akitolea mfano ziara ya hivi majuzi kuenda Pwani kwa ndege.

“Huwa nawatumia pesa na hata [mama] akitoka Nairobi nilimpa pesa na bado huwa nawatumia. Shida ya mama yangu anataka nikienda mahali kama Mombasa eti niende na yeye, na hilo halitowezekana,” Bradley alisema.

Kuhusu mwanamke anayedaiwa kuwa mke wake, Bradley alisema kuwa alimtoroka wakati hakuwa na pesa na sasa anataka kurudi kwa kujilazimisha kwake baada ya kuona nyota yake imeangaza tena.

"Ako, lakini sasa shida ya huyo msichana vile sikuwa na doh, akaamua kutoroka na vile tuliachana na yeye alienda kuoleka kwingine...sahii vile nimeanza kushika elfu tatu, nne, tano hivi, amesema sisaidii mtoto..na ashaolewa"aliongeza.

Awali katika klipu iliyowatia huruma wengi, mama mzazi wa Bradley alihojiwa akikiri kwamba mwanawe aliacha kuchukua simu zake tangu umaarufu kumjia mwezi mmoja uliopita.

"Bradley hata sahii nikipiga simu hashikii..wale manager ako wao wawili wamemshika..si rahisi anipigie simu..nilikuwa Nairobi, wakati mtoto alitoka Mombasa mara ya kwanza, hakuna siku alikanyaga mahali naishi.." mamake alisema.

 

View Comments