In Summary

• Pia, Bradley anasemekana kulamba dili nono la kuwa balozi wa mauzo katika chapa ya kampuni moja ya humu nchini ya kutengeneza unga.

BRADLEY MTALL
Image: FACEBOOK

Bradley Marongo ‘Mtall’ maarufu kama Gen Z Goliath amevaa suti kwa mara ya kwanza katika maisha yake.

Hii ni baada ya juhudi za chapa ya mavazi ya Bespoke City pamoja na Director Trevor ambaye alimuunganisha na muasisi wa chapa hiyo, Bolo Bespoke.

Trevor alimpeleka Bradley kwa Bolo Bespoke wiki kadhaa zilizopita na akaonekana akichukuliwa vipimo na kuahidiwa kushonewa nguo.

Kijana huyo alikiri kwamba katika maisha yake hajawahi vaa suruali ndefu wala viatu kutokana na kimo cha mwili wake ambacho kimefanya kuwa vigumu kwake yeye kupata viatu vinavyomtosha.

Baada ya kuchukuliwa viimo, wikendi iliyopita ilikuwa zamu yake kupokezwa zawadi yake adimu ya suti na Kaunda za kipekee ambazo zilionekana kumtoshea.

Akisherehekea zawadi hiyo mpya, Bradley alishukuru Trevor kwa kumshika mkono tangu siku ya kwanza na kumfanikishia ahadi hiyo.

“Mara ya kwanza katika suti, ninahisi mkali! Asante sana kwa Bespoke City kwa kunifaa na meneja wangu, Director Trevor kwa kufanikisha hilo,” Bradley alichapisha.

Kijana huyo tangu nyota ya jaha kumuangazia miezi miwili iliyopita wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z, amekuwa akipokea zawadi ainati, zingine zikiwa ni ahadi kutoka kwa watu mbalimbali.

Hivi majuzi, Mkurugenzi wa Bonfire Adventures, Simon Kabu baada ya kumfanikishia ziara ya siku chache kuelekea Pwani, alifichua kwamba kuna mtu kutoka taifa la Serbia ambaye amejitolea kumpa kijana huyo kazi nchini humo.

Pia, Bradley anasemekana kulamba dili nono la kuwa balozi wa mauzo katika chapa ya kampuni moja ya humu nchini ya kutengeneza unga.

View Comments