In Summary

• Marua alikiri kwamba hiyo ndiyo pete rasmi kwa ajili ya harusi yao akisema kwamba kwa mara ya kwanza alichafua kile kitu ambacho mwenyewe alikipenda.

•   “Pete ghali, Range Rover, jumba la kifahari, watoto wazuri.. kila kitu ni kwa juhudi za Bahati na nina deni lake kubwa.”

DIANA MARUA
Image: INSTAGRAM

Rapa Diana B amefichua kwamba pete yake ilimgharimu  mpenzi wake Bahati Kioko shilingi laki mbili za Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari za burudani, Marua alisema kwamba pete hiyo Bahati alimnunulia wakati wa kusherehekea miaka 7 ya uchumba wao na kwamba bei yake haikuwa ya laki moja na nusu bali ilikuwa ya 2ook.

“Hii pete yangu si ya sh170k kama mnavyosema, hata Bahati alisema ni Sh157k lakini ukweli ni kwamba bei yake halisi ni Sh200k,” Diana Marua alisema.

Akiwashauri watu wanaotazama video hiyo kutomzivia kwa ajili yak umkata kidole na kutoroka na pete hiyo, mama huyo wa watoto 3 alisema kwamba yeye anajijua ni mtu mwenye bahati sana maishani kwa kuwa na vitu vya bei ghali.

“Ambacho ninaweza kusema ni kwamba mimi ni mwenye bahati sana na mbarikiwa kwa kuwa nina mwanamume anayenipenda sana. Bahati kwangu ni kama ni mtu aliyetumwa kutoka mbinguni, kinadharia naweza sema alidondoshwa kutoka mbinguni.” Alisema.

Marua alikiri kwamba hiyo ndiyo pete rasmi kwa ajili ya harusi yao akisema kwamba kwa mara ya kwanza alichafua kile kitu ambacho mwenyewe alikipenda.

“Hii ndio pete rasmi kwa sababu angalau kwa mara ya kwanza nilichagua chenye nilipenda, sikuwa nataka aende anichagulie pete ambayo ingekuja ififie rangi na nivae nikitembea nayo na watu wananijua najiita ‘Auntie Madoh’. Hii tuliingia pale kwa duka, kulikuwa na aina mbalimbali lakini nilichagua hii na nikamwambia hii ndio nataka,” alisema.

Aliorodhesha baadhi ya vitu ambavy mume wake amemfanyia katika kipindi cha miaka 8 ya ndoa na kumshukuru kwa mapenzi yasiyojua kufa.

“Pete ghali, Range Rover, jumba la kifahari, watoto wazuri.. kila kitu ni kwa juhudi za Bahati na nina deni lake kubwa.”

View Comments