In Summary

• Butita pia alizungumzia jinsi ziara yake na rais Ruto kuelekea Marekani na hatimaye kufika katika ikulu ya White House kulimjengea uadui mkubwa na vijana wa Gen Z.

Eddie Butita akutanishwa na Steve Harvey.
Image: HISANI

Afisa mkuu mtendaji wa blogu ya SPM Buzz, Eddie Butita amefichua kwamba siku hizi yeye na staa wa televisheni kutoka Marekani, Steve Harvey ni marafiki na watani wakubwa.

Akizungumza na Oga Obinna, Butita alifichua kwamba tangu rais Ruto alimpomwezesha kukutana na Harvey mwezi Mei katika studio za Tyler Perry wakati wa ziara yake Marekani, wawili hao wamekuwa watani wakubwa kiasi kwamba wanatumiana meme za kuchekesha na kutaniani kwenye mtandao wa WhatsApp.

“Nilikutana na Steve Harvey. Huwa namuita Stevo, ni boy wangu. Tumezoeana na huwa tunatumiana memes. Hapo ndio imefika. Lakini mara ya kwanza nililia kuona nimekutana na Harvey ana kwa ana,” Eddie Butita alisema.

Butita pia alizungumzia jinsi ziara yake na rais Ruto kuelekea Marekani na hatimaye kufika katika ikulu ya White House kulimjengea uadui mkubwa na vijana wa Gen Z.

Alisema kwamba vijana wengi walimuona kama msaliti kwa vuguvugu lao la kumtaka rais Ruto kung’atuka mamlakani, kutokana na ukaribu wake naye ambao ulimuona akijumuishwa kwenye kundi la takribani watu 30 waliosafiri naye kwenda USA.

“Sijawahi ongelea ile ziara ya Marekani vizuri juu ‘nilizalimiwa’ baada ya hapo. Mimi nilikuwa nimetulia nikasikia niaje, rais ako na ziara na tunahitaji kuenda hadi studio za Tyler Perry kujifunza mawili matatu. Hivyo mimi nilikuwa pale kama msanii, si kama mwanasiasa. Lakini kwa bahati mbaya kuna watu waliona kama nilienda kama mwanasiasa. Lakini ninakubali kwa sababu Baraka hizo zilikuwa kubwa zaidi kwa baadhi ya watu kuzikubali,” Butita alieleza.

Alisema kwamba anafikiri kuna baadhi ya watu hawakuridhika na yeye kujumuishwa kwenye safari ya rais na walikuwa wanasubiri muda wa kutema nyongo yao, jambo ambalo walifanya wakati wa maandamano ya Gen Z.

View Comments