In Summary

• Ajib Gathoni afichua kuwa aliwahi fanya laiv moja na kupata 210k

• Pia amesema kuwa ana hali ya Adenomyosis na yuko katika matibabu.

• Miadi yake inayofuata ni Oktoba na anatarajiwa kurudi na maoni

Ajib Gathoni
Image: Instagram

Tiktoker Ajib Gathoni amefichua kuwa aliwahi kufanya TikTok live mara moja na kupata shilingi elfu 210.

Katika mahojiano yake na Mic Cheque Podcast alifichua kuwa hiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanya TikTok live ambayo aliifanya siku yake ya kuzaliwa na kwamba hajawai kuifanya tena.

2022 nadhani nilifanya live yangu ya kwanza siku yangu ya kuzaliwa...Katika muda wa dakika 3 nilipata 210k,” Ajib alisema.

Pia alizungumzia kuhusu hali yake ya  afya ya Adenomyosis ambayo alikuwa ameisema hapo awali.

Hivi majuzi Ajib alichapisha kuwa anaugua ugonjwa wa Adenomyosis.

“Niligunduliwa na Adenomyosis- hii ni hali ambapo ukuta wa mfuko wa uzazi hukua hadi kwenye misuli ya mfuko wa uzazi, Okay this is not harmful per se but it’s the one that causes the heavy and prolonged menstural bleeding and the severe cramping.”

Ajib alisema kuwa kwa sasa yuko kwa matibabu ili kutibu hali hiyo ingawa bado anaumwa.

So for starters nilipewa dawa ambazo nafaa kumeza chukua kabla ya siku zangu za hedhi na siku hizo pia. Miadi yangu inayofuata ni Oktoba na ninafaa kurudi na maoni…”Ajib aliandika.

Kulingana na Ajib, hali hiyo inatibiwa kutoweka kwa kutumia dawa sahihi, lishe bora na mazoezi.

View Comments