In Summary

•Bradley Marongo atembelea msemaji wa serikali Isaac Mwaura

•Wakenya wanaweza kupata vitambulisho ndani ya siku 10 kuanzia mwezi ujao

Bradley Mtall na Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura
Image: Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura, Bradley Mtall//Spokesperson GoK X

Jumanne msemaji wa serikali Isaac Mwaura alikutana na Bradley Marongo almaarufu Gen Z Goliath.

Leo mchana, Bradley Marongo almaarufu Gen Z Goliath au kwa ufupi ‘Bradley Mtall’, alitembelea ofisi ya msemaji wa serikali Isaac Mwaura,” Mwaura aliandika.

Wakati wa ziara hiyo, ilibainika kwamba Bradley hajapokea hati zozote muhimu za serikali ikiwa ni pamoja na cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha taifa.

Bradley alianza kupata umaarufu mtandaoni wakati wa maandamano ya kuipinga serikali kutokata na urefu wake wa kipekee.

Amekuwa gumzo mjini na kupata ufuasi mkubwa kutoka kwa mitandao ya kijamii.

Bradley amekutana na wasimamizi wa kampuni mbalimbali na kuweza kuwa balozi wa kampuni tofauti tofauti.

Msemaji wa serikali aliendelea na kusema kuwa wakenya sasa wataweza kupata vitambulisho ndani ya siku 10 kuanzia mwezi ujao.

Jumatatu, Julius Bitok , Katibu katika Wizara ya Uhamiaji na Huduma kwa Raia alithibitisha kwamba wakenya wanaohitaji vitambulisho  watapata hati hiyo ndani ya siku kumi.

Bitok alisema kuwa huo muda mfupi wa kusubiri utawezekana kwa kusambaza vifaa vya kukamata moja kwa moja katika vituo vya Huduma na ofisi za National Registration Bureau kaunti zote nchini.

Ufuatatilaji wa haraka wa vitambulisho pia utatokana na uwezo ulioimarishwa wa uchapishaji katika (National Registration Bureau) baada ya kupata vichapishaji viwili hivi majuzi.

View Comments