In Summary

 
• “Mbona sisi wenyewe tunazungumza tu, au tunawadangamnya sana nyie? Kuna lolote kumbe hamjui nyinyi?” aliongeza.

ALIKIBA NA DIAMOND
Image: HISANI

Bosi wa Kings Music, Alikiba kwa mara nyingine amesisitiza kwamba hana bifu lolote kati yake na mshindani wake wa muda wote, Diamond Platnumz.

Akizungumza na waandishi wa habari za burudani, Alikiba alisema kwamba hakuna ugomvi au pambano lolote la kibinafsi baina yake na Diamond na kusema ushindani wao unakuja kikazi tu.

Alikuwa anajibu kuhusu mdogo wake, Abdukiba kunekana kuanza kujenga ukaribu na Diamond na wasanii wake kama Mbosso.

“Kumuona Abdukiba na Mbosso pamoja hakuna jambo lolote ka kubarikiwa na mimi, sisi hatuna mapambano. Sisi ni kazi tu tunafanya na kazi zetu zinaposhindana basi ndio challenge inapotokea,” Alikiba alifafanua.

Msanii huyo alifichua kwamba anaelewa ukaribu wa hivi majuzi kati ya Abdukiba wa Kings Music na Mbosso kutoka WCB Wasafi, akisema kwamba ni marafiki kwa muda na hkuna ubaya kuhusu wao kuwa marafiki.

“Ninavyojua kuhusu Abdukiba na Mbosso, ni kwamba wao ni marafiki. Ni marafiki wa muda mrefu hata kabla Mbosso hajasainiwa kule, kuhusu kufanya kazi kwao, mimi huwa nabariki kazi zote za wasanii wangu, waniletee tu kazi nzuri. Ni nzuri tu ambayo pia mimi itaniingizia pesa, hicho ndicho hata mimi ninachotamani,” Alikiba alieleza.

Msanii huyo, bila kumtaja Diamond, alisema kwamba huwa wanazungumza tu lakini wanawadanya watu katika mitandao ya kijamii kwa kuigiza kuwa ni maadui wasioweza kupikika kwenye chungu kimoja.

“Mbona sisi wenyewe tunazungumza tu, au tunawadangamnya sana nyie? Kuna lolote kumbe hamjui nyinyi?” aliongeza.

View Comments