In Summary

• EP hiyo ilidokezwa kutoka mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Aprili na EP hii inajumuisha kiini cha uhakika wa sanaa hii yenye sura nyingi za msanii mwenye vipajii vingi.

• EP ya ‘Unstoppable’ inajumuisha ngoma 6 na moja ya nyongeza, zote zaikiwa ni utunzi wa kipekee wa binti huyo mrembo, SABRINA.

SABRINA
Image: HISANI

Sabrina, msanii chipukizi kutoka Kameruni ametangaza kuachia albamu mpya kwa jina ‘Unstoppable’.

Kupitia barua kwa vyombo vya habari, Sabrina aliweka wazi kwamba malengo yake katika albamu hiyo ni kuteka bara zima la Afrika na nguvu za Sanaa ya kiafrika kimuziki.

EP hiyo ilidokezwa kutoka mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Aprili na EP hii inajumuisha kiini cha uhakika wa sanaa hii yenye sura nyingi za msanii mwenye vipajii vingi.

EP ya ‘Unstoppable’ inajumuisha ngoma 6 na moja ya nyongeza, zote zaikiwa ni utunzi wa kipekee wa binti huyo mrembo, SABRINA.

EP hii ni barua ya mapenzi kwa Afrika; tofauti zake za kitamaduni, mandhari na maadili. Kila wimbo ni muunganiko wa midundo tofauti ya Kiafrika na sauti, inayoakisi utengamano wa Sabrina kama msanii asiye na kifani.

Mwaka jana, kwa ajili ya kumuenzi Yemi Alade wa Nigeria anayemtaja kama kichocheo kikubwa kwenye safari yake ya muziki, Sabrina alitoa Johnny, wimbo uliokuwa na jina sawa na wimbo ambao ulimfanya Alade kuwa maarufu mwaka wa 2013.

Ili kufikia hadhira pana zaidi, lugha ya Sabrina imelazimika kubadilika. Hapo awali, aliimba zaidi kwa Kifaransa, lakini sasa amekubali maneno zaidi ya Kiingereza.

Albamu yake ya ‘Unstoppable’ iliwekwa wazi kwa ajili ya ufikiaji na umma mnamo Juni 7 mwaka huu.

Tangu ajiunge na Afrobit Productions mwaka wa 2019, Mkameruni huyo ametoa nyimbo kadhaa, kama vile Validée, Catastrophe, La Don Go, na Five Star, ya mwisho ambayo ina za mtani wake Martin.

Albamu yake ya kwanza, Love Aganda yenye nyimbo tisa, ilitolewa mnamo Novemba 2021.

View Comments