In Summary

•Ringtone Apoko amewaita wasanii wa ngoma za kidunia kwa kukosa kuhudhuria hafla ya mazishi ya mamake Mr Seed

•Anataka wasanii wa Kenya kusaidiana na kuungana mkono jinsi wasanii wa Tanzania wanavyofanya

•Alikuwa anatoa hotuba hii akiwa katika hafla ya mazishi ya mamake Mr Seed

Ringtone.
Image: Instagram

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko amewaita wasanii wa ngoma za kidunia kwa kukosa kuhudhuria hafla ya mazishi ya mamake Mr Seed.

Katika hotuba yake kwenye mazishi, Ringtone alikashifu KRG na kusema kuwa huwa anajigamba na utajiri wake lakini alishindwa kuhudhuria hafla ya mazishi ya mama wasanii wenzake.

Ringtone alisema kuwa Cassypool na KRG wangeweza kumuonyesha Mr Seed uungaji wa mkono kwa kuhudhuria hafla ya mazishi.

KRG unajifanyanga uko na pesa kwa nini hungepata chopper ufike hapa? Cassypool unapiga mdomo Biashara Street kwa nini huwezi support wasanii?” Apoko aliuliza.

Ringtone aliendelea na kuwaita wasanii wa nyimbo za kidunia wakiwemo Khaligraph Jones, Nadia Mukami, Sauti Sol na wengine kwa kutosimama na Mr Seed huku akiomboleza marehemu mamake.Anawasihi wasanii wa Kenya kusaidiana na kuwaunga mkono wasanii wenzao jinsi wasanii wa Tanzania wanasaidiana.

Lazima wasanii wa Kenya tusaidiane na tusapotiane...Wasanii wa secular, Khaligraph, Nadia, nani...wote..mko wapi?...Sauti Sol, mko wapi?...lazima wasanii wa Kenya tuanze kusupportiana, Tanzania kitu ikifanyika woote unawaona Kenya hatusimami pamoja.” aliongeza.

Mamake Mr. Seed aliaga dunia Agosti baada ya kuugua kwa muda mrefu na baadaye akazikwa Septemba katika kaunti ya Siaya.

View Comments