In Summary

• Ali Kiba amewataka watangazaji wake, kwenye vipindi vyao kuhakikisha Bongo inatamba hewani.

Alikiba
Image: Instagram

Staa wa muziki wa bongo nchini Tanzania Alikiba ameamrisha vituo vya Crown Fm na Crown TV kucheza miziki ya Bongo Fleva kwa wiki moja mfululizo.

Staa huyo ambaye hivi maajuzi alizindua kituo hicho kilicho chini ya umilisi wake amewataka watangazaji wake, kwenye vipindi vyao kuhakikisha Bongo inatamba hewani.

Haya ni kwa mujibu wa mtangazaji Mwijaku wa kituo cha Crown Fm katika kipindi chake ambapo alikuwa akifanya mahojiano na Mkenya Cassypool.

Mtangazaji huyo alisema kuwa bosi wake alitoa mamlaka kwa kituo chake cha televisheni kuwa kicheze miziki ya kutoka Tanzania pekee kama hatua ya kukuza miziki kutoka nchi hiyo.

Aidha, Cassypool alimpongeza Ali Kiba akipigia mfano wa utofauti ulioko kati ya Kenya na Tanzania.

Cassypool alisema kuwa wacheza santuri (DJ) na wa presenta wa redio wanawakandamiza wasanii.

Kulingana na Cassypool, baadhi ya Wakenya wana roho chafu wasiojali taaluma ya wasanii. Cassypool aliwasihi Wakenya kuiga mfano wa Watanzania ambao wanajiweka kipaombele kabla ya kumfikiria jirani.

View Comments