In Summary

•Pia walielezea matatizo ambayo walipitia kabla ya Malaika kuzaliwa lakini kwa hayo yote walisema kuwa amekuwa zawadi kubwa katika maisha yao.

•Hii ni baada ya Bahati kusema katika mahojiano kuwa watamfichua mtoto wao baada ya siku kumi

Malaika Nyambura Bahati
Image: Malaika Bahati//HISANI

Wanamuziki Diana Marua na Kevin Bahati hatimaye wamefichua sura ya binti yao Malaika Nyambura Bahati.

Kwenye mahojiano ya hivi majuzi, Bahati alisema kuwa baada ya siku kumi, wangemfichua mwanao kwani wakishoot video ya 'The Bahati's Empire' alikuwa angali mdogo.

"Mashabiki wetu wa YouTube wamekuwa wakilalamika kwa sababu sio kila mtu yuko kwenye Nextflix na tunapanga kufichua rasmi labda katika siku 10 zijazo..Malaika uliyemuona kwenye Netflix alikuwa mtoto kwa sababu kipindi ilikuwa imerekodiwa mwaka mmoja uliopita,kwa hivyo mtamwona Malaika siku kumi zijazo. Hiyo sasa ni rasmi" Bahati alisema.

Tangazo la Jumatano halikuwa la kumuonyesha Malaika pekee bali pia walielezea matatizo ambayo walipitia kabla ya Malaika kuzaliwa lakini kwa hayo yote walisema kuwa amekuwa zawadi kubwa katika maisha yao.

"Lakini ninachoweza kusema ni kwamba Malaika amekuwa baraka kubwa katika maisha yetu...baraka kuu katika maisha yetu," Diana alisema.

Diana pia alisema kuwa wataonyesha mashabiki jinsi Malaika amekuwa tangu utotoni mpaka sasa alipo.

"Safari yake ya kukua ilikua safari nzuri na nadhani baada ya muda tutakuwa tunashare nanyi jinsi safari yake imekua akikua, akiwa mdogo hadi alipo sasa hivi," Diana aliongeza.

Diana na Bahati walimkaribisha mtoto wao Malaika mnamo November 1, 2022 na kuchagua kutoonyesha uso wake.

Baadaye walimfichua mara ya kwanza kwenye kipindi chao Netflix, 'The Bahati's Empire' lakini mashabiki wengi walilalamika kuwa hawajaweza kumuona kwa sababu hawapo kwenye Netflix, jambo ambalo lilipelekea ufunuo wa pili Jumatano Septemba, 2024.

Bahati, Baby Malaika, Diana
Image: Bahati,Malaika,Diana//HISANI
View Comments