In Summary

• “Bebi? Unajua sasa hivi wewe si Bebi… piga simu uone jina ambalo linakuja,” Dem wa FB alimwambia Obinna akimtaka kupiga simu.

• Wiki chache zilizopita, Obinna alimsindikiza Dem wa Facebook kuelekea nyumbani kwao kaunti ya Trans Nzoia na kuandaa sherehe ya kipekee kumkaribisha mrembo huyo nyumbani.

OBINNA NA DEM WA FB
Image: HISANI

Mkuza maudhui chipukizi, Dem wa Facebook amefichua jinsi amekuwa akibadilisha majina anayotumia kuhifadhi nambari ya simu ya rafiki na bosi wake, Oga Obinna.

Wawili hao ambao wamekuwa wakitengeneza maudhui pamoja kupitia Obinna TV wameonyesha ukaribu wao, Obinna akimiminiwa sifa kwa kumshika mkono mrembo huyo chipukizi aliyeanza kama mchekeshaji na kumuongoza kwenye safu ya utengenezaji maudhui.

Katika kipindi chao cha hivi karibuni, Dem wa FB alimfichulia Obinna kwamba ameshabadilisha jina alilokuwa anatumia kuhifadhi namba yake na kusema kwamba sasa anamtambua kama ‘dhahabu’ – My Gold.

“Bebi? Unajua sasa hivi wewe si Bebi… piga simu uone jina ambalo linakuja,” Dem wa FB alimwambia Obinna akimtaka kupiga simu.

“Wewe huoni, acha nionyeshe kamera watu ndio waseme. Mumeona, nimemhifadhi ‘My Gold’. Wewe ni dhahabu yangu kwa sababu dhahabu ni vitu ghali zaidi. Wewe ni dhahabu yangu,” Dem wa Facebook alimwambia.

Haya yanakuja siku chache baada ya Obinna kumnunulia gari la kwanza Dem wa Facebook kama zawadi.

Wiki chache zilizopita, Obinna alimsindikiza Dem wa Facebook kuelekea nyumbani kwao kaunti ya Trans Nzoia na kuandaa sherehe ya kipekee kumkaribisha mrembo huyo nyumbani.

Awali akianza kutengeneza maudhui naye, Obinna alimzawadia Dem wa FB na simu mahiri ya iPhone, baada ya kusutwa kwa kuomba mashabiki kuchanga pesa za kumnunulia simu hiyo.

View Comments