In Summary

• Mrembo huyo ambaye pia ni vixen kwenye video za miziki ya wasanii alifichua kiasi kikubwa ambacho amewahi pokea ni milioni 20 za kitanzania kutoka kwa Marioo.

SOHSOLAITI AISHA FERUZY
Image: INSTAGRAM

Aisha Feruzy, mwanasosholaiti anayeibukia kwa kasi nchini Tanzania amedai kwamba kando na kuwa na bima ya maisha, pia ana bima nyingine ambayo ni mahususi kwa ajili ya makalio yake.

Mrembo huyo mwenye makalio makubwa ambayo yanawanyima usingizi wanaume wengi, haswa wasanii wa Bongo Fleva, alifichua hili kupitia mahojiano ya kituo cha redio cha Times FM.

Alikiri kwamba ana mpenzi ‘mubaba’ ambaye kando na kumkatia bima ya maisha, pia amemkatia bima spesheli kwa ajili ya makalio yake, akisema kwamba yeye hupenda sana kufurahia maisha mazuri.

“Mubaba wangu ananipenda sana, warembo siku hizi tunapenda sana wababa kwa sababu wababa ni watu wanaotujali sana. Mfano kama mimi, mubaba wangu amenifanyia vitu vingi sana. Mfano amenikatia bima ya maisha, mimi nimekatiwa hadi bima ya makalio. Kama litatokea lolote, nitalipwa,” mrembo huyo alisema.

“Ikatokea kwa mfano mtu kanichoma sindano vibaya nikavimba, nitalipwa. Ikatokea nikaenda sehemu nikajikwaruza kidogo nitalipwa. Bima hiyo ipo na analipa hela nyingi sana – milioni 3 kwa mwezi,” aliongeza.

Kuhusu shepu lake, Feruzy alifafanua kwamba yeye hajatengeneza bali anatumia dawa na yupo kwenye mlo maalum kwa ajili ya urembo wake.

“Mimi sijatengeneza shepu kusema kweli, mimi natumia dawa. Kuna dawa natumia kwa ajili ya tumbo. Hutengenezi, unakuwa tu umejitunza vizuri. Dawa zinapunguza kitambi, zinaongeza nyama kwenye makalio. Mimi nachukia wanawake wenye vitambi,” alisema.

Mrembo huyo ambaye pia ni vixen kwenye video za miziki ya wasanii alifichua kiasi kikubwa ambacho amewahi pokea ni milioni 20 za kitanzania kutoka kwa Marioo.

“Kazi ya mwisho ambayo nimefanya ni ‘Yule’ ya Marioo na AY. Na walinilipa milioni 20 [pesa za kitanzania]. Nafikiri walichanga. Na sikufanya vipengele vyote. Mimi ili kuonekana kwenye video yako gharama yangu kuanzia milioni 20 kwenda juu,” alifafanua.

 

View Comments