In Summary

• Aliomba Mungu kuongoza hatua za binti Malaika wakati ambapo anaanza safari ya kuonyesha maisha yake kwenye mitandao ya kijamii.

• Hata hivyo, miaka miwili baadae, anapiga tathmini nyuma na kumlaani ibilisi akidai kwamba ndiye alikuwa kazini kusababisha hayo yote.

BAHATI NA MKEWE WAKATI WA MIMBA YA MALAIKA.
Image: INSTAGRAM

Rapa Diana B amesimulia changamoto ambazo alipitia wakati wa ujauzito wake wa mwanawe wa tatu, Malaika Bahati.

Kupitia ukurasa wake, saa chache kuelekea utambulisho rasmi wa Malaika Bahati kwenye jamii ya mitandaooni, Diana Marua alifichua kwamba haikuwa safari rahisi kubeba ujauzito wa binti huyo.

Diana alifichua kwamba alikuwa Analia aghalabu na kwa wakati mmoja kulikaribia kusababisha kuvunjika kwa ndoa yake, huku akifichua kwamba aliwahi toroka ndoa yake wakati anapitia makuruhu ya ujauzito huo.

Hata hivyo, miaka miwili baadae, anapiga tathmini nyuma na kumlaani ibilisi akidai kwamba ndiye alikuwa kazini kusababisha hayo yote.

“Safari yangu ya ujauzito haikuwa rahisi. Tulikuwa na siku ngumu. Nililia sana, nilihama nikiwa mjamzito sana, Uhusiano wangu ulikaribia kusambaratika. Ibilisi alikuwa kazini! Kusema kidogo, ILIKUWA MBAYA!!!” Diana alisema.

“Hata hivyo, Mungu alijionyesha. Alirejesha kwetu siku za huzuni kwa kicheko, Alitujalia amani ipitayo ufahamu wetu wenyewe na kupitia hili, naweza kushuhudia kwamba Mungu hufanya kazi kwa njia zake mwenyewe za siri,” aliongeza.

Aliomba Mungu kuongoza hatua za binti Malaika wakati ambapo anaanza safari ya kuonyesha maisha yake kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunapomtambulisha rasmi Mtoto wetu Malaika kwa ulimwengu, Mungu… Ninaomba kwamba umlinde na kumuongoza dhidi ya chochote ambacho si chako. Ninaamuru na kutangaza kwamba hakuna mamlaka yoyote dhidi yake itafanikiwa, ninaomba kwamba daima atatembea katika Fadhili zako, Neema na Upako wako. Ataitwa Mwenyeheri Kati ya Mataifa na kwamba atapata Upendeleo kwa wanadamu na Mbinguni. Katika Jina la Yesu Ninaomba, AMEN,” alihitimisha kwa mtindo wa maombi na kusujudu.

 

View Comments