In Summary

• Kuna wanaume wanaolipa shilingi elfu kumi ili kupata nambari yangu ya simu sawia na muda wa kula chamcha na wao.

• Kimani anasema kuwa ni rahisi mwanamume kuondoka akiambiwa alipe pesa kuliko kumwambia nina mtu tayari.

Media Personality Deyanah Kimani
Image: IG//deyanah_kimani

Mtangazaji Deyanah Kimani amekiri kuwa anawalipisha wanaume shilingi elfu kumi ili kuwapa nambari yake ya simu.

Kimani alisema kuwa ni vigumu kummwambia mwanaume anayetaka kuwa na mahusiano hapana hivyo basi kulipisha nambari ya simu ni njia rahisi ya kumkwepa.

Kulingana na mwanahabari Kimani ni kuwa wanaume wengi ni vigumu kukubali wanapoambiwa na wasichana wanaowataka kuwa wapo kwenye mahusiano au wana wapenzi tayari.

"Wakati unamwambia mwanamume unataka namba yangu aya nipe kapa kumi(elfu kumi)  hatakubali." Alisema Deyanah.

Kutokana na kulipisha namba, Kimani anasema kuwa wanaume wengi huwa hawakubali kumlipa ili kuwa na namba yake.

Aidha mwanahabari huyo alikiri kuwa kuna wanaume ambao wanalipa shilingi elfu kumi ili kupata nambari yake ya mawasiliano.

Kw wale wanaolipa, Kimani alisema kuwa urafiki huendelea katika mazungumzo kwa sababu huwa amelipiwa kwa wakati wanazungumza kupitia simu.

Mazungumzo yanapozidi kuendelea wakati mwingine yeye huenda kupata chakula cha mchana na mwanamume aliyepata namba yake kwa malipo hayo.

"Naweza enda kula chamcha na wao, lakini pia nalazimika kutafuta wakati huo ambao lazima watalipia kwa sababu mimi si bidhaa ya bure. Hiyo ndio shida." Alisema Deyanah Kimani.

 

View Comments