In Summary

•Felicity Shiru anatafuta nyumba ya kuishi baada ya kuhama mahali alipokuwa anaishi awali

•Anataka nyumba yenye vyumba viwili ama vitatu vya kulala

Felicity Shiru
Image: Felicity Shiru//Facebook

Muundaji maudhui Felicity Wanjiru almaarufu Felicity Shiru anatafuta nyumba ya kuishi baada ya kutoka mahali alipokuwa anaishi hapo awali.

Katika video yake ya YouTube, aliambia mashabiki wake kuwa anatafuta nyumba na kuwa kuna kitu maalum ambacho anatafuta.

“Nitakuwa natafuta nyumba leo na kuna kitu maalum ninachotafuta...I prefer staying in a stand alone rather than an apartment...si ati apartment ni kitu mbaya or anything...personally I feel like I want that space,” alisema

Anataka nyumba yenye vyumba viwili au vitatu vya kulala kwa kuwa ana mtoto,yaya na mgeni yeyote ambaye atamtembelea.

“Mungu akipenda, nitapata stand alone pengine vyumba viwili au vitatu vya kulala..Tutakuwa tunaishi hapo mimi ofcourse Zoey and the nanny and sometimes naweza have some visitors,"

Kuhusu mahali anataka kuishi alisema kuwa hataki kuishi Thika Road lakini anapendelea mjini ama pande za Kiambu.

“Area nataka kuishi I'm not quite sure coz siwezi jilimit lakini si Thika Road...Napendelea kukaa karibu na mji ama pande za Kiambu,”

Felicity alikuwa anaishi na Thee Pluto eneo la Thika Road na inasemekana aliondoka baada ya wao kutengana.

Hivi majuzi Thee Pluto alitangaza kuvunjika kwa uhusiano wake wa kimapenzi na mpenzi wake Felicity Shiru.

Kupitia Instagram, Pluto alichapisha ujumbe akithibitisha kusambaratika kwa ndoa yake iliyodumu kwa miaka 3.

Aliomba mashabiki wake kuheshimu faragha yao wakati huu ambapo kila mmoja wao ameamua kujishughulisha na hamsini za kwake.

‘Tumeamua kila mmoja kufuata njia yake na hivyo kufikisha mwisho uhusiano wetu uliodumu kwa miaka mitatu. Ahsante kwa sapoti yenu kutoka kwa familia, marafiki na mashabiki. Hebu na tusije tukaanza kushuku chochote na kuanza kusambaza uvumi usio wa kweli kuhusu utengano wetu,” Thee Pluto alitangaza.

Baada ya Felicity kutengana na mpenzi wake Thee Pluto, ilifichuliwa kuwa amekuwa akikaa na mamake.

Felicity na Thee Pluto wana mtoto mmoja msichana anayejulikana kama Zoey.

View Comments