In Summary

• Kasmuel amesema amepokea jumbe nyingi kwenye simu yake kutoka kwa watu mbali mbali wanaomfuatilia wakimtaka kuweka wazi ikiwa amejiunga na serikali.

• McOure amewahakikishia watu wanaouliza ikiwa amenunuliwa kuwa hajanunuliwa na sasa kazi anayofanya haimweki katika rubaa za kitaifa.

Mwanaharakati Kasmuel McOure Akishiriki maadamano jijini Nairobi
Image: X//Kasmuel McOure

Mwanaharakati Kasmuel McOure ameomba radhi wafuasi wake kwa kuonekana akicheka na mbunge Silvanus Osoro katika picha na video iliyosambaa mtandaoni.

McOure  amesema kwamba anajutia kukubali kupiga picha na mjumbe.

 Kasmuel amesema kuwa amepokea jumbe nyingi kwenye simu yake kutoka kwa watu mbali mbali wanaomfuatilia wakimtaka kuweka wazi ikiwa amejiunga na serikali.

"Sijafanya kazi na serikali, nimepata ofa mara nyingi na nimefikiwa mara nyingi tangu tulipoanza maandamano."  Alisema Kasmuel.

McOure hata hivyo ameeleza kuwa jibu lake limesalia kuwa hana hamu ya kufanya kazi na serikali.

"Sina hamu ya kufanya kazi na serikali wakati inaendelea kuwaua watu wetu."  Alisema McOure.

Kulingana na McOure, picha iliyosambaa mtandaoni ilipigwa na mbunge wa kike aliyekuwa ameandamana na mbunge Osoro.

Mwanaharakati huyo alisema kuwa alikuwa hajawai kutana na MP Osoro na hapo ndipo waligundua kuwa wanashiriki katika kanisa moja.

Wakati walipokutana, Kasmuel McOure alikiri kuwa  alimweleza Osoro  anachohisi kuhusu jinsi wanavyoendesha serikali yao wahuni.

Aidha amewahakikishia watu wanaouliza ikiwa amenunuliwa kuwa hajanunuliwa na sasa kazi anayofanya haimweki katika rubaa za kitaifa.

 

View Comments