In Summary

• Ng’ang’a alisema kwamba hakukaa kinyonge, kwani aliwasindikiza nje na neno akiwataka wasiwahi rudi.

PASTA NG'ANG'A
Image: HISANI

Mchungaji wa kanisa la Neno Evangelism, James Maina Ng’ang’a amefichua kwamba alipoteza idadi kubwa ya waumini wa kike katika kanisa lake wakati alipomtambulisha mke wake kanisani.

Akizungumza katika ibada kwenye video moja ambayo imekuwa ikienezwa katika mitandao ya kijamii, Ng’ang’a alifichua kwamba wanawake wengi waliondoka kanisani pindi alipomtambulisha mke kwao, kwani wengi wao walikuwa wanatarajia angewaoa wao.

“Mke wangu yuko hapa. Nilipotaka kumuoa, kulitokea kizungumkuti sana, hili kanisa lilikuwa limejaa kote na wanawake wengi sana. Wengi walikuwa wanani’approach kwa sababu ukiwa na upako na uko na pesa, wanawake kwako ni kama matope tu, yaani wako kila mahali….”

“Sasa nilipoitana tu akatangazwa ndiye mchumba, niamini ninapowaambia wanawake waliamka 700 wakati uo huo na kuondoka. Walikuwa wamejua mke wangu wa kwanza si amefariki, hata wale ushers waliondoka wakisema ‘sasa hawezi hata tufikiria’. Nilipoteza zaidi ya waumini 4,000,” Ng’ang’a alisema.

Ng’ang’a alisema kwamba hakukaa kinyonge, kwani aliwasindikiza nje na neno akiwataka wasiwahi rudi.

“Na mimi nilisimama nikawaambia muende kabisa, mke ni wangu si wa Mungu. Wengine walisema eti mke wangu ni mtoto, na mimi nikauliza ni mtoto kwani mnakula eti hamtashiba? Ni wa kuuza eti pesa hazitarudi?” Ng’ang’a aliongeza.

View Comments