In Summary

•Sandy Kahush anasema kuwa wanaume wanafaa kuangaliwa vizuri kwa sababu ni viumbe dhaifu

SANDY KAHUSH
Image: INSTAGRAM

TikToker Sandy Kahush anasema kuwa wanaume wanafaa kuangaliwa vizuri kwa sababu ni viumbe dhaifu.

Katika mahojiano na Oga Obinna, Sandy alisema kuwa wanawake wanapaswa kuwatunza waume wao vizuri kwa sababu mwanamume ambaye anaangaliwa vizuri nyumbani hataenda kuhanya.

Alipoulizwa sababu ya wanaume kukosa uaminifu kwenye mahusiano alisema kuwa ni wanawake ndio sababu kwani anapo mtunza mwanaume vizuri hana haja ya kukosa uaminifu kwenye mahusiano.

“Wewe ndio sababu yake[mwanamke]…Nikuulize you get that treatment usiku, you get that treatment asubuhi your woman is always there for you would you cheat?,” aliuliza.

Aliongeza kuwa huenda mwanaume akakosa uaminifu kwenye mahusiano, mke anafaa kumuuliza kile ambacho alifanya kibaya na kutatua tatizo hilo. “Unamuuliza ulikosea wapi,”

Sandy alisema kuwa huenda mwanamume akamkosea ama kutoelewana na mwanamke, anafaa kukalishwa chini na kuongeleshwa kwa upole.

Anasema kuwa mwanamke akiwa mzuri mwanamume atamskiza, “Ukiwa mzuri kwa mwanamume atakuskiza.”

Kahush anasisitiza kuwa wanawake wanafaa kutengea wanaume wao wakati na kutekeleza majukumu yao vizuri.

Kwa mahojiano yake ya hivi karibuni na Commentator 254 Sandy alisema kuwa anaweza mfanyia mwanamume wake chochote iwapo ako katika nafasi ya kumfanyia kitu.

"Kama wewe ni mwanamume wangu, nitakufanyia kila kitu.Kama niko nayo nitakupea hata naweza kununulia hiyo gari kama niko nayo,” Sandy alisema.

View Comments