In Summary

•Alisema baadhi ya waimbaji wa injili na alipoulizwa kusema ni nani bora zaidi, alimtjaa Guardian Angel.

•"Nimemfahamu tangu anaanza kwenye tasnia, na tumekuwa pamoja katika hafla mbalimbali." alisema.

Image: INSTAGRAM// GUARDIAN ANGEL

Mwimbaji wa nyimbo za injili wa Tanzania Rose Muhando amemtaja Guardian Angel kama msanii anayempenda zaidi wa nyimbo za Injili kutoka Kenya.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi majuzi akiwa nchini Kenya, Muhando aliombwa kuzungumzia waimbaji anaowapenda zaidi.

Alisema baadhi yao na alipoulizwa kusema ni nani bora zaidi, alimtjaa Guardian Angel.

"Nyimbo zao zote ni nzuri. Size 8 ambaye nina wimbo naye, Betty Bayo, Solomon Mukubwa na Guardian Angel," alisema.

Muhando aliongeza kuwa anamfahamu Guardian kwa muda mrefu na kwamba atafurahi kufanya naye kazi.

"Nampenda Guardian Angel na jinsi anavyoimba. Mtindo wake wa uimbaji, kuna ladha anayoweka kwenye nyimbo zake," alisema.

"Nimemfahamu tangu anaanza kwenye tasnia, na tumekuwa pamoja katika hafla mbalimbali."

Alipoiona video hiyo, Guardian Angel alijibu, akisema amenyenyekea, na kuongeza kuwa anatumai mwaka huu watafanya kazi pamoja.

"2023 Mungu awezeshe."

Size 8 alipofanya collabo na Muhando, alisema wimbo huo ulitoka mioyoni mwao kuthamini zawadi ya maisha baada ya kupigana vita tofauti maishani.

“Nimetamani kufanya collabo na msanii nguli tangu nilipookoka miaka saba iliyopita,” alisema.

Mama huyo wa watoto wawili aliongeza kwamba waliungana haraka.

"Tuliifanya haraka sana. Muda mfupi zaidi ambao nimewahi kufanya kazi kwenye wimbo wowote na mtu yeyote. Neema ya Mungu ilitosha sana. Ana uzoefu sana."

View Comments