In Summary

•XXX Tentacion alipigwa risasi nyingi shingoni katika tukio linalodaiwa kuwa la wizi huko Deerfield Beach, Florida.

•Pop Smoke alipigwa risasi akiwa nyumbani kwake Hollywood Hills, Marekani katika tukio linaloshukiwa kuwa la uvamizi wa nyumbani na wizi.

Image: INSTAGRAM// TAKE OFF

Jumanne, habari za kusikitisha kuhusu kifo cha rapa maarufu Takeoff wa kundi la Migos zilivunja mioyo ya walimwengu, hasa wapenzi wa Hip hop.

Takeoff ambaye ndiye mdogo zaidi kati ya wanabendi watatu wa Migos aliripotiwa kufariki baada ya kupigwa risasi Jumanne asubuhi wakati wa mchezo wa kete ambao alikuwa amehudhuria na mwenzake Quavo ambaye pia ni mjomba wake.

Duru za kuaminika zilisema kuwa tukio hilo lilitokea Houston, Marekani muda mfupi baada ya saa nane unusu asubuhi ya Jumanne baada ya kutokea ugomvi kati ya washiriki wa mchezo huo ambapo risasi kadhaa zilifyatuliwa na kumpata Takeoff. Alitangazwa kuwa amefariki papo hapo katika eneo la tukio.

Takeoff alifariki akiwa na umri wa miaka 28. Maelfu ya walimwengu wakiwemo watu mashuhuri wameeleza kusikitishwa kwao kufuatia tukio hilo. Wengi bado wanaendelea kutuma risala zao za rambirambi kwa familia na kundi la Migos.

Takeoff hata hivyo sio rapa wa kwanza mashuhuri kuuawa kwa risasi katika miaka ya hivi majuzi. Chini hapa kuna marapa wengine maarufu ambao walipoteza maisha yao kwa risasi na matukio yaliyozingira mauaji yao:-

Jahseh Dwayne Ricardo Onfroy (XXX Tentacion) - Juni 18, 2018 (Miaka 20)

XXX Tentacion alipigwa risasi nyingi shingoni katika tukio linalodaiwa kuwa la wizi huko Deerfield Beach, Florida.

Ermias Joseph Asghedom (Nipsey Hussle) - Machi 31, 2019 (Miaka 33)

Hussle alipigwa risasi takriban mara 10 katika maegesho ya gari ya duka lake lililo Los Angeles. Mauaji yake yalidaiwa kuchochewa na suala la kati yake na muuaji.

Bashar Barakah Jackson (Pop Smoke) Februari 19, 2020 (Miaka 20)

Rapa huyo alipigwa risasi akiwa nyumbani kwake Hollywood Hills, Marekani katika tukio linaloshukiwa kuwa la uvamizi wa nyumbani na wizi.

Adolph Robert Thornton Jr (Young Dolph) - Novemba 17, 2021 (Miaka 36)

Dolph alikuwa akinunua vitafunwa katika duka moja katika mji wa Memphis, Marekani wakati mtu mwenye bunduki alipoendesha gari hadi alipokuwa, akapiga risasi na kumuua kupitia dirishani.

Rakim Hasheem Allen (PNB Rock) - Septemba 12, 2022 (Miaka 30)

Rapa PnB Rock alifariki dunia baada ya kupigwa risasi akiwa anakula kwenye mgahawa na mpenzi wake katika tukio lililoonekana kama wizi uliolengwa.

Dayvon Daquan Bennett (King Von) - Novemba 6, 2020 (Miaka 26)

Rapa King Von alifariki baada ya makabiliano makali nje ya klabu ya usiku ya Atlanta ambayo yaliishia kwa vita vya risasi.

View Comments