In Summary

•Msanii huyo mwenye umri wa miaka 30 aligura tasnia ya injili takriban miaka mitatu iliyopita huku akiitaja kama ‘iliyooza’.

•Mwaka wa 2021, alifichua kwamba alifunga siku kadhaa kabla ya kugura injili na kuanza kuimba nyimbo za mapenzi.

Bahati
Image: INSTAGRAM

Kuna uwezekano kwamba mwimbaji Kelvin Kioko almaarufu Bahati anatafakari kurejea kwa ghafla kwenye muziki wa injili.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 30 aligura tasnia ya injili takriban miaka mitatu iliyopita huku akiitaja kama ‘iliyooza’.

Siku ya Jumapili, Bahati kwenye ukurasa wake wa Instagram alichapisha tena video ya sehemu ya wimbo wake 'Barua' iliyochapishwa kwenye Tiktok ambapo mchapishaji alisema wanamkosa sana akiimba injili.

Chini ya chapisho hilo, baba huyo wa watoto watano aliwauliza mashabiki wake aina ya muziki wanayotaka kutoka kwake,

"Je, mnatamani zaidi kutoka kwa huyu Bahati wa zamani (Mwimbaji wa Injili) au Bahati wa sasa?" Bahati aliuliza.

Mamia ya wanamitandao walijumuika chini ya chapisho la mwimbaji huyo na kutoa maoni yao kuhusiana na hatua hiyo.

djshiti_comedianKabisa

kiragumaureen Bahati wa barua kabla ya Marua.

wangechi. tabby Nakumbuka nilikuwa nimekukufia na nilikuwa najua nyimbo zako zote. Hata sasa bado nakupenda.

jay_maimah Siku hizo maisha yalikuwa rahisi na nafuu. Siku hizi maisha ni magumu ata ukiimba hizo nyimbo za awali hazitatuingia kwa hivyo kaa mahaili uliko.

chebet_songok Tunapenda wa sasa lakini pia tunamkosa wa kitambo.

Bahati alitangaza kugura injili mwaka wa 2020 lakini akaweka wazi kuwa imani yake kwa Mungu haikuwa imepunguka hata kidogo.

Mwanamuziki huyo alifichua hayo wakati wa mahojiano na mchekeshaji MC Jessy kwenye kipindi chake Jessy Junction.

“Injili ni Kristo. Nina Kristo moyoni mwangu na ninaamini katika Mungu na Mungu ndiye sababu ya mimi kuwa kileleni hivyo siwezi kumwacha Kristo,’’  alisema.

Alidai kwamba tasnia hiyo imeoza na kuweka wazi kuwa uamuzi wa kugura ndio bora zaidi ambao aliwahi kufanya.

“Nilipigwa vita sana katika tasnia ya injili lakini nilijua sifanyi muziki wa injili kwa ajili ya watu; Nilikuwa nikifanya kwa ajili ya Mungu.

Nimejitenga na tasnia ya injili kwa muda lakini si kutoka kwa Mungu. Kristo na Bwana ndiye mwokozi wangu binafsi,” alisema.

Mwaka wa 2021, alifichua kwamba alifunga siku kadhaa kabla ya kugura injili na kuanza kuimba nyimbo za mapenzi.

View Comments