In Summary

•Lupita alimtambulisha mtangazaji wa televisheni Selema Masekela kama mpenzi wake  kupitia video nzuri ambayo alipakia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. 

"Mioyo imeshikamana. Mpenzi wangu kamili na halisi @lupitanyongo❤❤❤," Selema aliandika.

Muigizaji mashuhuri wa Hollywood Lupita Nyong'o hatimaye amemtambulisha mpenzi wake hadharani kwa mara ya kwanza.

Lupita ambaye ni binti wa gavana wa Kisumu Anyang' Nyongo alimtambulisha mtangazaji wa televisheni Selema Masekela kama mpenzi wake  kupitia video nzuri ambayo alipakia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. 

Katika video hiyo, wapenzi hao walionekana wakiwa wamevalia mavazi tofauti yanayofanana huku wakicheza kwa vidole vyao.

"Tunaingiana tu 💖 @selema #thisismylove  #nuffsaid, (Huyu ni mpenzi wangu, yamesemwa ya kutosha," Lupita aliandika chini ya video hiyo fupi ambayo alichapisha kwenye  Instagram siku ya Ijumaa.

Selema ambaye ni mtangazaji na mwimbaji wa Marekani alithibitisha kuwa Lupita Nyong'o ni mpenzi wake wa kweli.

"Mioyo imeshikamana. Mpenzi wangu kamili na halisi @lupitanyongo❤❤❤," aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Selema Masekela , 51, ni mwandishi wa habari za michezo na pia ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya mavazi  ya Mami Wata.

Mwezi Aprili 2022, Lupita (39)  aliungana na mpenzi huyo wakekatika uzinduzi wa kampuni  hiyo yake  iliyo Venice, California.

Hapo awali, Lupita alihusishwa na Black muigizaji wa Black Panther Michael B. Jordan. Kabla ya hapo, pia ilidaiwa kuwa alikuwa akichumbiana na muigizaji Jared Leto baada ya wawili hao kuwa karibu mwaka wa 2014. Baadae hata hivyo,  Nyong'o alifafanua kuwa wana urafiki wa karibu tu, 

Maelfu ya wanamitandao wakiwemo watu mashuhuri wamewapongeza Lupita na Selema baada ya kutangaza mahusiano yao.

@janellemonae Nimependa 😍😍

@elainewelteroth Mapenzi yanashinda ❤❤❤❤ Na ndio hivyo! Nawapenda nyote hadi kwenye mwezi

@daniebb3 Hii inapendeza zaidi

@juniornyongo 👑👑👑👑👑

@mstialawson taja wanandoa wazuri zaidi kuliko hawa

View Comments