26 November 2015 1 Min Read
Zaidi ya nusu ya vijana wanaoishi na HIV wanapata matibabu
by Brian Ndungu Habari
Picha kwa hisani ya: ruralreporters
Zaidi ya nusu ya vijana wanaoishi na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi wanaweza kufikia matibabu.
Celestine Ndinda kutoka baraza la kuthibiti maambukizi ya ukimwi anasema asilimia 42 ya vijana wanaoishi na HIV wanatumia dawa za kupunguza makali huku akiongeza kwamba kuna umuhimu wa wote kutumia dawa hizo ili kupunguza idadi ya wale wanaoaga dunia.