Nchi ya Botswana imefutilia mbali sheria ya enzi za ukoloni iliyoharamisha   mapenzi ya jinsia moja  katika kesi kubwa  iliyokuwa ikifuatiliwa na watu wengi barani afrika .

Uamuzi huo wa Botswana unajiri  siku chache tu baada ya Kenya hivi maajuzi kutilia mkazo msimamo wa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja .

Mahakama kuu jijini Gaborone  imesema sheria iliyokuwa ikitoa adhabu kali kwa ushoga na mapenzi ya jinsia moja wa jumla  ilikuwa  kinyume na katiba .

View Comments