Botswana yafutilia mbali sheria inayoharamisha mapenzi ya Jinsia moja

 

 Nchi ya Botswana imefutilia mbali sheria ya enzi za ukoloni iliyoharamisha   mapenzi ya jinsia moja  katika kesi kubwa  iliyokuwa ikifuatiliwa na watu wengi barani afrika .

Uamuzi huo wa Botswana unajiri  siku chache tu baada ya Kenya hivi maajuzi kutilia mkazo msimamo wa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja .

Mahakama kuu jijini Gaborone  imesema sheria iliyokuwa ikitoa adhabu kali kwa ushoga na mapenzi ya jinsia moja wa jumla  ilikuwa  kinyume na katiba .