Eneo la mkasa wa mlipuko wa trela la mafuta Morogoro ,Tanzania

Takriban watu 57 wameafariki  katika mlipuko wa trela la kubeba mafta nchini  Tanzania ,polisi wamesema . Picha zilizowekwa mtandaoni  zinaonyesha moto mkubwa ukiteleteza sehemu  kubwa ya eneo huku miili yenye majeraha ya moto ikitapakaa kote .

Ripoti ambazo hazina  ithibati zinasema kwamba  atu walikuwa wakijaribu kufyonza mafuta  kutoka kwa gari hilo ambali lilibingiria wakati  mlipuko ulipotokea . Kisa hicho  kimefanyika Morogoro yapata kilomita 200 magharibi mwa Jiji la Dar es salaam .

Mji wa morogoro ni kitovu muhimu cha usafirishaji wa mafuta  kutoka bandari ya Dar .Kuna hofu kwamba idadi ya walioangamia huenda ikaongezeka .

View Comments