‘Mat of death’:DCI Yawanasa wahudumu wa matatu waliomwua abiria kwa kumsukuma .
Idara ya DCI imewakamata wahudumu wawili wa matatu waliomsukuma abiria kutoka gari lililokuwa mbioni na kumwua . Polisi wamesema gari hilo nambari ya usajili KCC 021A limenaswa kufuatia kifo cha Gerald Kimondo. Wawili hao Naphtali Fondo mwenye umri wa miaka 33 na Alex Gikonyo mwenye umri wa miaka 20 walimsukuma mwendazake kutoka gari hilo lililokuwa mbioni na kusababisha kifo chake .
Kisa hicho kiliripotiwa kutokea agosti tarehe mbili mwaka huu katika barabara kuu ya Thika karibu na Roysambu baada ya abiria huyo kutofautiana na washukiwa hao wawili . Kimondo aliaga dunia papo hapo baada ya kusukumwa . kondakta wa basi hilo alitorka baada ya tukio hilo lakini basi lenyewe likanaswa na dereva kukamatwa .Baadaye dereva aliachiliwa huru baada ya siku mbili katika hali ya kutatanisha . Ilidaiwa aliachiliwa huru kwa bondi ya polisi yenye thamani ya shilingi elfu 60 pamoja na basi hilo kwa jina zam zam .
OCPD wa Kasarani Peter Kimani alipoulizwa kuhusu kuachiliwa kwa dereva huyo na basi ,alisema liliondolewa hatia . “ Utaratibu wa trfaiki ni kuwa gari linaposababisha ajali ,ukaguzi unafanywa na kisha linaachiliwa .lakini kesi hiyo inaendelea’ amenukuliwa akisema OCPD huyo .