Naomi Ireri afunguka A-Z alivyougua ukimwi kwa tendo moja la ndoa
Mwanadada kwa jina la Naomi Ireri, 41, amefunguka jinsi tendo la ndoa mara moja lilimpa virusi vya ukimwi.
Akizungumza na kituo cha utangazaji nchini, Naomi alishiriki kimapenzi na mwanaume aliyemwacha baadaye.
"Niligundua nilikuwa na virusi vya ukimwi nikiwa na miezi mitano katika vipimo vya kliniki...
"Nilidhani nilikuwa sawa ila siku moja nikapimwa katika hospitali ya kibinafsi na kuitishwa damu yangu..."
"Walichukua (wahudumu) muda mrefu kuniita na nikaanza kujiuliza mbona wengine wanaitwa ndani na sio mimi..." alisimulia Naomi.
Naomi aliamua kwenda ndani ili aongee na muhudumu,
"Wakati nilipoingia daktari aliniuliza, ushawahi kupimwa virusi vya ukimwi? Na nikasema sijawahi...'
"Hapo ndipo niliambiwa kuwa nina virusi vya ukimwi..." Naomi.
Taarifa za kuugua maradhi ya ukimwi zilimshtua zaidi Naomi,