NICE HAIR! Vyakula bora kwa nywele yenye afya .Fahamu unachohitaji kula kwa nywele nzuri
Kitu cha kwanza ambacho hukutangaza kama mtu ni nywele ,na hasa kwa akina dada . ni muhimu kufahamu jinsi unavyoweza kuwa na nywele ndefu na yenye afya kutumia vyakula bora ambavyo vitakunufasha kuboresha afya ya nywele yako . Kando na mafuta na kemikali nyingi zinazotumiwa kwa ukuuzaji na utunzi wa nywele ,vyakula hivi pia ni muhimu sana na havina madhara ya kando ambayo hutokana na matumizi ya kemikali au mafuta ya kutunza nywele .
1. Mayai
Mayai ni kitovu muhimu cha protini na biotin ,virutubiusho muimu sana katika ukuaji wa nywele . kula protini ya kiasi kifaacho ni muhimu kwa ukuaji wa nywele .ukosefu wa protini umefahamika kusababisha kupotea kwa nywele . biotin ni muhimu sana kwa utenezaji w protini muhimu kwa jina keratin .
2.Tunda dogo/ Berries
Matunda madogo ya Berries yamejaa viungo na vitamini muhimu vya kuwezesha ukuaji wa nywele . vitamin hizo ni pamoja na Vitamin C . Mwili huyumia vitamin C kutengeza kiungo cha collagen ,protini ambayo hufanya nywele kuwa thabiti na kuizuia kuchanika . Vitamin C pia huusaidia mwili kupata madini ya chuma au Iron kutoka kwa vyakula .uhaba wa Iron husababisha ugonjwa wa Anaemia ambao husababisha kupotea kwa nywele .
3. Spinach
Mboga ya spinach ina madini muhimu sana yanayowezesha ngozi kutoa unyevu na vitamin A na C ambazo husaidia ktika ukuaji wa nywele . ufuta maalum kwa jina Sebum hutolewa na ngozi ya kichwa ili kusaidia katika ukuaji wa nywele . Gramu 30 za spinach hutoa takriban aislimia 54 ya mahitaji yako ya kila siku ya Vitamin A .
4. Samaki wa ufuta
Samaki wenye ufuta kama vile Chache au salmon husaidia katika ukuaji wa nywele .samaki hao hutoa omega 3 ambazo ni aside zinazohusishwa na ukuaji wa nywele . Mafuta ya samaki pia huzuia kupotea kwa nywele na kuongeza ukuaji wa nywele kwa wanawake .
5. Viazi vitamu
Viazi vitamu ni muhimu sana kwa madini ya beta-carotene. Mwili hubadilisha kiungo hiki muhimu kuwa Vitamin A ambavyo vinahusishwa na afya nzuri ya nywele . Kiazi kimoja kitamu kina takriban gramu 114 za beta carotene inayoweza kukupa vitamin A mara nne zaidi ya mahitaji yako ya kila siku .
6. Parachichi/Avocados
Avocados ni tamu sana na zina mafuta ya jani ya kiasini ambayo yana vitamin E inayosaidia sana katika ukuaji wa nywele .Vitamin E pia hulinda sehemu ya ngozi kama vile nyozi ya ufuvu wa kichwa . avaocado pia zina aside maalum yenye mafuta ambayo huzuia nyewele kupotea . Vyakula vingine muhimu katika ukuaji wa nywele yenyeafya ni Njugu ,Pilipili tamu ,chaza/Oysters,uduvi/shrimp,maharagwe,soya na nyama.