Watu watano wamefariki  katika eneo la  Kighombo huko  Mwatate mkaunti ya Taita Taveta baada ya maporomoko ya ardhi  kuivunika nyumba yao kufuatia mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo . Waliofariki ni  Mwanamme mmoja ,mkewe na watoto wao watatu . Miili ya mwanamme huyo,mkewe na mtoto mmoja imepatikana huku juhudi za  kuitafuta miili miwili ya watoto wao wengine ikiendelea .

Kamishna wa kaunti hiyo Rhoda Onyancha  amewatahadharisha wakaazi wa Voi na sehemu nyingine zilizo katika hatari ya kukumbwa na maporomoko ya ardhi kuhamia maeneo  yenye miinuko yaliyo salama .

 

View Comments