Watu watano wamefariki katika eneo la Kighombo huko Mwatate mkaunti ya Taita Taveta baada ya maporomoko ya ardhi kuivunika nyumba yao kufuatia mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo . Waliofariki ni Mwanamme mmoja ,mkewe na watoto wao watatu . Miili ya mwanamme huyo,mkewe na mtoto mmoja imepatikana huku juhudi za kuitafuta miili miwili ya watoto wao wengine ikiendelea .
Kamishna wa kaunti hiyo Rhoda Onyancha amewatahadharisha wakaazi wa Voi na sehemu nyingine zilizo katika hatari ya kukumbwa na maporomoko ya ardhi kuhamia maeneo yenye miinuko yaliyo salama .