Chupa

 Kuanzia jumamosi  itakuwa hatia kuwa na maji au kinywaji  cha chupa kisichokuwa na muhuri maalum wa ushuru mpya. Huenda utakamatwa na kushtakiwa kwa kukwepa kulipa kodi endapo utapatikana na bidhaa hizo bila mhuri maalum.

Hii ni kwa sababu  muda wa miezi mitatu uliotolewa kwa watengezaji wa bidhaa, waagizaji, wauzaji na wananchi  kufuata sheria mpya ya utozaji kodi bidhaa hizo utatamatika siku ya Ijumaa Januari tarehe 31.

Bidhaa hizo zote sasa zinafaa kubandikwa stempu maalum  wakati wa kutengezwa zinapopakiwa kwa mujibu wa kanuni hizo mpya za KRA . Watengezaji wote na waagizaji wa bidhaa hizo sasa wanahitajika kuafikia  kanuni hizo  kwa bidhaa zote zinazoingizwa nchini baada ya Novemba tarehe 13  mwaka wa 2019  na zile zisizokuwa na stempu maalum za kulipa ushuru huo mpya   zinafaa kuwasilishwa kwa afisi iliyo karibu ya kodi kufikia Januari tarehe 31 mwaka wa 2020.

View Comments