Kuanzia jumamosi itakuwa hatia kuwa na maji au kinywaji cha chupa kisichokuwa na muhuri maalum wa ushuru mpya. Huenda utakamatwa na kushtakiwa kwa kukwepa kulipa kodi endapo utapatikana na bidhaa hizo bila mhuri maalum.
Hii ni kwa sababu muda wa miezi mitatu uliotolewa kwa watengezaji wa bidhaa, waagizaji, wauzaji na wananchi kufuata sheria mpya ya utozaji kodi bidhaa hizo utatamatika siku ya Ijumaa Januari tarehe 31.
Bidhaa hizo zote sasa zinafaa kubandikwa stempu maalum wakati wa kutengezwa zinapopakiwa kwa mujibu wa kanuni hizo mpya za KRA . Watengezaji wote na waagizaji wa bidhaa hizo sasa wanahitajika kuafikia kanuni hizo kwa bidhaa zote zinazoingizwa nchini baada ya Novemba tarehe 13 mwaka wa 2019 na zile zisizokuwa na stempu maalum za kulipa ushuru huo mpya zinafaa kuwasilishwa kwa afisi iliyo karibu ya kodi kufikia Januari tarehe 31 mwaka wa 2020.