kakamega primary

Baadhi ya wanafunzi  walionusurika  katika kisa cha mkanyagano katika shule ya msingi ya Kakamega  kilichosababisha vifo vya wenzao 14 wamedai kwamba mwalimu mmoja alikuwa akiwafukuza  waondoke  shuleni  baada ya masomo jioni . Hata hivyo  haijatolewa taarifa rasmi ya kueleza sababu ya kisa hicho  ambacho kimewatamausha wengi .

Wazazi waliowapoteza wanao wamefurika katika hospitali ya rufaa ya kakamega  ili kuitambua miili ya watoto wao . Waziri wa elimu  George Magoha  ,katibu wa kudumu Belio Kipsang  na gavana wa Kakamega  Wycliffe Oparanya  walizuru shule hiyo siku ya jumanne asubuhi ili kutathmini hali . Wengine  waliozuru  shule hiyo  ni seneta wa kakamega Cleophas Malala , seneta wa zamani wa kaunti hiyo  Bony Khalwale  na msemaji wa serikali  Cyrus Oguna .

View Comments