kUTTUNY

  Kulikuwa na patashika katika boma la  mbunge wa cherangany Joshua Kutuny mtaani Hardy wakati mwanamke mmoja alipowasili huko akidai kwamba mbunge huyo amemtelekeza mtoto waliyezaa naye .

Joyline Chemutai  anadai kwamba  mbunge huyo hajakuw aakituma pesa za kumsaidia mwanawe . Polisi wamesema walipewa taarifa kuhusu kizaazaa katika boma la mbunge huyo mwezi wa  saa sita usiku .

Polisi waliojibu tukio hilo walielekea kwa Kutuny na kumpata mwanamke huyo akipiga kelele . katika  patashika hiyo afisa mmoja wa polisi kwa jina Emmanuel Maiyo alifyatua risasi hewani ili kuleta utulivu .

 

View Comments