Kulikuwa na patashika katika boma la mbunge wa cherangany Joshua Kutuny mtaani Hardy wakati mwanamke mmoja alipowasili huko akidai kwamba mbunge huyo amemtelekeza mtoto waliyezaa naye .
Joyline Chemutai anadai kwamba mbunge huyo hajakuw aakituma pesa za kumsaidia mwanawe . Polisi wamesema walipewa taarifa kuhusu kizaazaa katika boma la mbunge huyo mwezi wa saa sita usiku .
Polisi waliojibu tukio hilo walielekea kwa Kutuny na kumpata mwanamke huyo akipiga kelele . katika patashika hiyo afisa mmoja wa polisi kwa jina Emmanuel Maiyo alifyatua risasi hewani ili kuleta utulivu .