- cannibal
- idi aziz
- masauti
- brown mauzo
- wasanii (1)

Wasanii wengi wanaoshikilia hadhi ya burudani ya humu nchini huku muziki wao ukiskizwa nchini kote, Afrika mashariki na hadi ulaya.

Baadhi ya wasanii hawa wanatambulika kwa ubabe wao kuanzia zama zile kwa mfano Nyota Ndogo na Cannibal, ila sio wengi wanaojua wasanii wa kizazi kipya.

Wasanii hawa wametuwezesha kushindana na wasanii wa Bongo huku baadhi yao wakijizolea tuzo chungu nzima.

Nyota ndogo

Kwa miongo kadhaa, Nyota Ndogo amekuwa akitesa kimziki na baadhi ya nyimbo anazatambulika nazo ni 'Nibebe' akimshirikisha Nonini pamoja na 'Watu na viatu'.